Pata Msaada wa Ushuru Bila Malipo

Msaada wa kuwasiliisha ushuru ambao ni salama rahisi na bila malipo.

Okoa dola zako nyingi ulizochuma kwa bidii na upate msaada bila malipo wa kuwasilisha ushuru wa mwaka wa 2020.

Kuanzia Januari. 20-Aprili. Wataalamu 18 wa ushuru ambao wamefundishwa mwaka huu wa 2021 na kudhibitishwa na IRS, watakuwako kukupatia msaada wote asilimia 100 wa kuwasilisha ushuru wako kupitia mtandao. Wataalamu wetu wanajua sheria zote mpya za ushuru na mikopo inayopatikana, kutia ndani zilizoko kwenye mswada mpya wa misaada, ili kukuwezesha kuongeza faida zako na kuhifadhi pesa zako zaidi. Pia tunaweza kukusaidia kudai pesa za hundi ya kichocheo (stimulus cheque).

Msaada bila malipo wa kuwasilisha ushuru unatolewa kwa kila mtu, kutia ndani wamiliki wa ITIN.

Ili tuweze kukusaidia kwa njia bora zaidi na ushuru aako, hapa kuna vitu vichache ambavyo utahitaji kutia ndani na hati zingine ambazo si lazima, lakini ukikusanya na kuwa nazo, zinasaidia:

Unachohitaji

  • Kadi ya Kitambulisho ambayo ina picha yako
  • Picha yako ukiwa umseshika kadi hiyo ya kitambulisho karibu na uso wako
  • Kadi ya Usalama wa Jamii(Social Security Card) au hati ya ITIN
  • Hati zozote za kuonyesha mapato yako (kama vile W-2, 1099-R, na zinginezo)

Hati Zingine Ambazo Si Lazima Kuwa Nazo

  • Hati ya ushuru wa mwaka uliyopita
  • Taarifa ya Soko la Bima ya Afya (1095-A)
  • Taarifa ya Utunzaji wa Watoto
  • Taarifa ya Ushindi wa Kamari
  • Taarifa ya Malipo ya Karo

Njia Rahisi ya Kujaza Ushuru Bila Malipo


Pata mtu akusaidie

GetYourRefund.org

Pata huduma za kutayarisha ushuru bila malipo kupitia mtandao. Wataalamu waliodhibitishwa na IRS watafanya kazi pamoja na wewe kutayarisha marejeo yako ya ushuru na kuiwasilisha kielektroniki kupitia mtandao. Tovuti ambayo ni salama inatumika kukusaidia kutuma hati zinazohitajiwa kwa urahisi.

Wasilisha mwenyewe

MyFreeTaxes.com

Kupitia MyFreeTaxes.com, unaweza kuwasilisha ushuru wako mwenyewe bila malipo. Ili kutumia huduma hii utahitaji kutengeneza akaunti, halafu ujaze na kuwasilisha ushuru wako mwenyewe.

Piga simu upate msaada

2-1-1

Unaweza kupiga simu 2-1-1 kupata habari na msaada katika lugha mbalimbali, kutia ndani msaada wa kujua jinsi ya kuwasilisha ushuru wako bila malipo.


Asante kwa Wafadhili Wetu: